Inavyofanya Kazi
Huo ni Mfano
Mtu Yeyote Anaweza Kuifanya
- Zumbua chaneli yetu na uone kile kinachopatikana. Hakikisha hukosi orodha ya mpangilio wa video kwenye YouTube ambayo inakusaidia kuzingatia video za masomo na maswali tu.
- Tengeneza mpango wa jinsi unavyotaka kuzitumia video, iwe darasani, kwa mafunzo binafsi, au kwa mafunzo ya nyumbani. Hapa kuna ratiba ya mwongozo wakujifunza ambayo tumetengeneza kama mfano ili upate kuanza. Ikiwa utatumia video zetu kujifunza Kiebrania siyo lazima kutumia kitabu. Ikiwa unataka kutumia kitabu, unaweza, lakini ni chaguo lako kabisa.
- Fanya mazoezi ya kusema maneno na misemo kwa sauti, kwa sababu kufanya hivyo kutakusaidia kuingiza lugha na ujisikie unaimiliki. Tazama video tena na tena kama unavyohitaji mpaka utaanza kuelewa.
- Jitahidi kuzoea kusoma kama mtoto. Hiyo inamaanisha ukubali utata kwa muda mfupi.
- Usikose video za majaribio baada ya kila masomo machache ambazo hukupa fursa ya kufanya mazoezi kwa sauti na kuona unavyoendelea. Unaweza kushangazwa ni kiasi gani umejifunza baada ya video chache tu! Hata ikiwa huwezi kukumbuka msamiati wote kwenye jaribio, usijali! Ikiwa unaweza kuukumbuka, vyema, lakini jambo muhimu zaidi ni kwamba unalitambua na kulielewa neno wakati unapolisikia.
- Hakikisha unatazama masomo kwa mpangilio, kwa sababu katika kila somo linalofuata ni mwendelezo wa somo lililopita na tunadhani unajua tayari msamiati na sarufi iliyofundishwa kwenye video zilizopita.
Videkezo Saba kwa Kujifunza Lugha za Kibiblia
MOJA. Tengeneza kadi ya maombi ambayo itakusaidia kuomba juu ya masomo yako mara kwa mara. Sawa na kipengele kingine chochote cha kumfuata Yesu, kusoma Kiebrania na Kiyunani pia kunahitaji maombi. Adui hataki watu wawe na silaha ya upanga wa Roho Mtakatifu (yaani Neno la Mungu, Waefeso 6:17), kwa hivyo omba kwa bidii na usome kwa bidii! Hapa kuna baadhi ya vitu ambavyo navipendekeza vya kuandika kwenye kadi yako ya maombi, pia nitaviandika kwenye maelezo ya video hii hapa chini. Timotheo wa Kwanza 4:15 inasema “Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote.” Kwa hivyo njia ambayo ningeomba mstari huu itakuwa, “Baba, nisaidie kutekeleza mambo ninayojifunza, nijizamishe ndani yao, ili wote wapate kuona maendeleo yangu.”
Hapa kuna mistari mingine ya kuweka kwenye kadi: “Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.” (2 Tim 2:15). “Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana wala si kwa wanadamu.” (Kol 3:23). “Namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi.” (Rum. 12:3). “Mwende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo.” (Efe. 4:1-2). Mwishowe, ni pamoja na mawaidha yafuatayo kutoka kwa John Newton, mwandishi wa wimbo “Neema ya Kushangaza”: “Maandiko ya asili yanastahili maumivu yako, na yatawalipa sana.”
PILI. Pata mwenza wa kusoma ikiwa utaweza. Uwajibikaji ni muhimu, hasa wakati unapofanya kozi unayojiongoza mwenyewe kwenye mtandao. Ni kanuni rahisi ya kibiblia: wawili ni bora kuliko mmoja. Mwenza wako anaweza kukielewa kitu vizuri zaidi na kuweza kukusaidia; na kinyume chake. Mnaweza kutiana moyo wakati mambo yanapokuwa magumu.
TATU. Jifunze kidogo kila siku. Watu wengi hufanya makossa ya kufikiria wanahitaji tu kiasi kikubwa cha wakati/muda mara moja kwa wiki, lakini ubongo wako haufanyi kazi hivyo kwa kujifunza wa lugha. Ni bora kusoma dakika 20 kwa siku kila siku kuliko masaa 4 mara moja kwa siku moja. Polepole na thabiti hushinda mbio katika kujifunza lugha za kibiblia. Mwanzoni hautaona mrejesho kwa kiasi kikubwa kwa uwekezaji wako, lakini ikiwa utakaa sawa na kujenga tabia ya kusoma mara kwa mara, utafikia hatua wakati utakapoanza kuvuna mavuno makubwa kwa bidii yako.
NNE. Pata usingizi mwingi. Kuna kitabu kizuri kinachoitwa Kwanini Tunalala ambacho kinazungumza juu ya jinsi ilivyothibitishwa na masomo ya kisayansi kwamba tunahitaji kulala ili kuingiza habari mpya. Tunapolala kidogo, ndivyo tunavyoweza kujifunza na kuhifadhi kidogo. Ili ubongo wako ufanye kazi vizuri, unahitaji kuhakikisha unapata angalau masaa nane ya usingizi mzuri kwa usiku.
TANO. Sikiliza sana lugha kwa kadiri iwezekanavyo, hata ikiwa huelewi mambo mengi. Tunapendekeza programu hii ya bure iliyoundwa na idara ya mafunzo ya Kiebrania ya SIL Papua New Guinea. Programu inatoa sauti ya msomaji mtaalamu ambaye hutumia matamshi sawa na video za Aleph na Beth, na unaweza kupunguza kasi ya sauti katika programu ikiwa unataka. Kadiri unavyosikiliza zaidi, ndivyo utakavyoweka ndani sauti, mdundo, na ladha ya lugha. Hii itakusaidia kuendelea kuona Kiebrania kama lugha hai, ambayo itafanya uzoefu wako wa kujifunza uwe wa kupendeza na wa kuhamasisha. Pia, mfichuo zaidi wa sauti na mifumo ya lugha unayo, mambo mengi “yatasikika” au “kuhisi” sawa au vibaya kwa asili, hata ikiwa haujui sheria halisi kwa kumbukumbu.
SITA. Kuwa sawa na utata. Sehemu kubwa ya kujifunza lugha halisi ni kujifunza kuelewa kinachoendelea kutoka kwa vielelezo vya kuona na muktadha, hata ikiwa huelewi kila undani wa maneno unayoyasikia. Unapokuwa katika mchakato wa kujifunza, usizingatie sana kuchimba kila undani wa sarufi halafu kukosa kufuata mtiririko wa lugha na mazungumzo. Ruhusu maswali yako yakae na wewe kwa muda kidogo badala ya kudai jibu haraka. Kurudia zaidi na kuona na kusikia msamiati na miundo ya kisarufi mara nyingi kutajibu maswali yako, na wakati mwingine utagundua kuwa umeingiza muundo au neno bila hata kufahamu kabisa! Kwa maneno mengine, wacha ubongo wako wa kujifunzia lugha ufanye kazi yake kwa muda, na usisumbuliwe sana kwa kuzingatia sana juu ya maelezo madogo unapoanza ikiwa yanakuzuia kuingiza na kufurahia mtiririko wa lugha mpya.
SABA. Kuwa mnyenyekevu. Moja ya majaribu makubwa ambayo utakumbana nayo wakati wa kujifunza lugha za kibiblia ni kiburi, haswa kiburi cha kiroho. Ikiwa haujajiandaa kuvunja kiburi ndani ya moyo wako kila siku na kukikanyaga mpaka kitakapovunjwa kama mende, usijifunze lugha za kibiblia. Ujuzi wa Kiyunani au Kiebrania hutumiwa mara nyingi kama muundo wa kidini kutufanya tuonekane wa kiroho zaidi ya kweli tulivyo, kufunika dhambi zetu zingine ili wengine watusifu.
Jambo jingine ambalo linaambatana na kuwa mnyenyekevu ni: Kuwa mwangalifu usiwe mjinga mwenye hekima. Sisi wanadamu tuna tabia ya kufikiria sisi ni wenye hekima wakati sisi ni wapumbavu kweli. Inakwenda na msemo “Kujifunza kidogo ni jambo hatari.” Hiyo haimaanishi kuwa huwezi kujifunza kidogo. Inamaanisha tu kwamba unapaswa kukaa mnyenyekevu na kujikumbusha wakati wote kwamba hujui sana. Kwa watu wengi ambao hawajui mengi, ni ngumu sana kutambua ni kiasi gani hawajui, kwa hivyo fahamu hilo. Pia, wale ambao ni wajinga wana tabia zaidi ya kukosoa wale ambao kwa kweli wanajua mengi. Kwa hivyo unapojifunza lugha, kuwa mwangalifu usijifikirie mwenyewe zaidi kuliko inavyostahili! Lakini badala yake fikiria mwenyewe kwa busara (Rum 12:3).
Kwa Matumizi Bila ya Mtandao
Ikiwa ungependa kushirikisha video zetu kwa wengine ambao wana mtandao mdogo au hawana, au unataka tu kuwa na video bila ya mtandao, video hapa chini inaelezea jinsi utakavyoweza kufanya hivyo kwa urahisi.