kuliwezesha Kanisa la ulimwengu kwa utafsiri wa Biblia na zaidi

Kiebrania cha bure. Milele.

Kiebrania inaweza kuwa ghali, inaweza kuogopesha, na kukuchanganya. Tunataka kubadilisha jambo hilo.

Tunaunda rasilimali za mafunzo za bure za Kiebrania ili kuwasaidia watafsiri wa Biblia ulimwenguni kote na pia kujenga Kanisa la ulimwengu, ambao wengi wao wana uwezo mdogo wa lugha za asili za Bibilia au hawana uwezo kabisa.
 
Faida
wanafunzi wako kote ulimwenguni
0 +

Njia yetu inaweza kumsaidia yeyote kwa lugha yoyote.

Mapendekezo

"Kujifunza Kiebrania cha Biblia sio lazima kuwa ngumu au kuwa na gharama kubwa. Katika video hizi nzuri, utaongozwa katika mafunzo yako kwa kuonyeshwa kwa kurudiarudia pamoja na vitu vya kuchezea na picha. Hakuna Kiingereza kinachohitajika. Video hizi zinapendekezwa sana!"
"Wanafunzi wa huduma za kanisa, wachungaji na waamini wanamtafuta huyo mwalimu wa Kiebrania hapatikani ambaye anaweza kuifanya lugha hiyo kuwa ya kufurahisha, na kuvutia, na kukumbukwa. Sijui njia bora ya ufundishaji kuliko njia hii ambayo ni video za Aleph na Beth. Video hizo ziko bure, fupi, zina ubora wa juu sana, na zinatumia njia ya "lugha hai" kufundisha. Furahia video hizo, na ushangae jinsi unavyoweza kufahamu lugha ya Kibiblia kwa haraka!"
"Aleph na Beth ni njia nzuri ya kujifunza Kiebrania! Upendo wa Beth kwa Kiebrania unawavuta wengine. Natamani ningekuwa na masomo haya ili kuongeza ufanisi katika masomo yangu ya Kiebrania ambayo yalifundishwa kwa muundo wa kizamani. Ninapendekeza masomo haya kwa kutumia mtandao kwa wanafunzi ambao nimewafundisha zamani na pia kwa wanafunzi wapya. "
"Aleph na Beth ni rasilimali nzuri ambayo ninapendekeza sana. Video hizi za elimu zilizoundwa vizuri ni za ubunifu na ni nyepesi kuzielewa. Zinasaidia kujifunza Kiebrania bila kuogopa na badala yake kufurahisha sana! Nimetumia video za Aleph na Beth katika darasa langu la Kiebrania la Kibiblia katika Tyndale Seminary ili kusaidia mafundisho ninayotoa darasani. Rasilimali hii bora ni zawadi nzuri, na ninawashukuru Bethany na Andrew kwa bidii zote walizozifanya kutuandalia masomo haya mazuri. Todah rabbah. Asante."

Angalia wanafunzi wanasemaje...