Kuhusu Sisi

Maono yetu

Sisi huko Aleph na Beth tunaamini kwamba lugha za kibiblia zinaweza na zinapaswa kuwa kawaida mpya kwa uanafunzi. Kwa muda mrefu, kujifunza Kiebrania na Kiyunani imekuwa kitu kinachotengwa kwa ajili ya wachungaji, viongozi na makuhani, na kwa wale watu walio na pesa za kulipia masomo ghali ya lugha. Hii imesababisha ujuzi wa lugha za kibiblia kuhusishwa na “wasomi wa kiroho” wenye elimu. Lakini sasa tunaishi katika wakati ambao haujawahi kutokea wakati Mungu ametupa zana mpya na teknolojia ya kuzifanya lugha za kibiblia zipatikane kwa kila mtu ulimwenguni — bure! Unaweza kusoma zaidi juu ya falsafa yetu ya rasilimali za bure hapa.

Watu wengi ambao wameamua kujifunza Kiebrania cha kibiblia hawafikii malengo yao, na wale wachache wanaoweza kujifunza, wanapata shida kuhifadhi na kutumia kile walichojifunza. Ukweli ni kwamba, watu wengi ulimwenguni hawakuundiwa kujifunza lugha kwa kutumia kitabu cha maandishi na kukariri sheria (rules of language) nyingi. Badala yake, tunajifunza lugha bora kwa kuitumia: kuisikia na kuizungumza. Kila mtu ana uwezo aliozuliwa nao, aliopewa na Mungu wa kujifunza lugha kwa njia ya asili waliyojifunza kuzungumza lugha yao ya mama wakiwa watoto: kwanza kusikiliza, kuelewa, kuzungumza kidogo kidogo, halafu alfabeti na sheria za sarufi. Aleph na Beth wanakaribisha mtindo huu wa asili, mtindo wa kukutumbukiza katika kujifunza, na polepole kujenga ufahamu wako unapoangalia video. Njia hii ya asili ya kujifunza lugha inafurahisha, na kuwa bora zaidi baada ya muda kupita, wakati sauti na sarufi ya Kiebrania cha Bibilia zinapofanya kazi kwenye kumbukumbu yako ya muda mrefu kupitia kurudia na kutumia.

Katika ulimwengu wa magharibi tuna “aibu ya utajiri.” Tuna maelfu ya rasilimali za kibiblia ambazo zinapatikana mara moja tu, na kwa lugha tunayoelewa vizuri. Lakini, wakati huo huo, kuna mamilioni ya watu katika nchi zingine ambao hawana hata Biblia katika lugha yao mama. Kwa hivyo lengo letu ni kuliwezesha kanisa la ulimwengu kuelewa lugha za kibiblia, na pia kufundisha watu ambao watahusika katika utafsiri wa Biblia. Kwa kufanya hivyo, video zetu zinapaswa kupatikana kwa urahisi kwa kadiri iwezekanavyo kwa mtu yeyote wa lugha yoyote ili mtu asipaswe kujifunza kwanza Kiingereza halafu baadaye ajifunze Kiebrania. Ndio sababu hutawahi kusikia maelezo kwa Kiingereza katika masomo yetu ya video. Utajifunza Kiebrania kupitia… Kiebrania! Wakati huo huo, tunafanya kazi kuunda rasilimali za sarufi za ziada na kushirikiana na watu wanaojitolea kote ulimwenguni ili kuzitafsiri rasilimali hizo katika lugha kuu halafu kila mtu ataweza kupata zana anazohitaji kuelewa Kiebrania vizuri.

Tunakualika ujiunge nasi katika safari hii ya kuelekea katika lugha ya Biblia ya Kiebrania! Angalia masomo yetu yanayofurahisha na yanayozamisha kwa chaneli yetu ya YouTube.  Usisahau kujiandikisha ili usikose masomo ya hivi karibuni, na tafadhali washirikishe na marafiki kutoka nchi zingine na wanaoongea lugha zingine wanaopendezwa kujifunza Kiebrania! Pia tafadhali jisikie huru kupakua video na rasilimali zetu na kusambaza nje ya mtandao kwa wale walio na uwezo mdogo wa kupata mtandao. Wale walio na uwezo mdogo wa kupata mtandao ni wale ambao tunataka kuwawezesha zaidi.

!תּוֹדָה רַבָּה

Sisi ni Nani

Beth (Bethany) kila wakati alikuwa akipendezwa na lugha mbalimbali tangu alipokuwa mtoto (unaweza kuangalia daftari lake la lugha linaloshangaza kutoka wakati alipokuwa anasoma sekondari hapa). Ana kipaji ya kufanya sanaa (unaweza kuona sanaa yake kwenye Instagram yake hapa). Mapenzi yake yalimwongoza kupata masomo ya Isimu kutoka Chuo Kikuu cha North Dakota, na sasa anasoma PhD katika Kiebrania cha kibiblia kupitia Chuo Kikuu cha Free State nchini Afrika Kusini. Alitumikia kwa miaka mitano huko Kolombia akifundisha wamishonari wa baadaye vitu kama Upataji wa Lugha ya Pili na Fonetiki. Baada ya hapo alienda kusoma Kiebrania katika Kituo cha Watafsiri wa Biblia cha Jerusalem, ambapo alikutana na Andrew.

Je! Vipi kuhusu Andrew? Kwa kifupi, yeye ni mshauri wa tafsiri ambaye ameandika miziki mingivitabu vichache, ametengeneza programu za maombi, anaendesha podcast, na aliwahi Guinea ya Ikweta. Sasa yeye na Beth wanaishi na kufanya kazi Oaxaca, Mexico ambapo Andrew alikulia. Jisikie huru kutufuata kwenye Facebook hapa.

Shalom!