Kwanini Njia Yetu?
Maudhui Yanayoeleweka
Kuiweka Rahisi
Sema Kwaheri kwa Msongo wa Mawazo
Kanuni nyingine muhimu ya kujifunza lugha ambayo Stephen Krashen anazungumzia ni kwamba lazima kusiwe na msongo wowote wa mawazo katika mchakato wa kujifunza. Ikiwa wanafunzi wanajisikia kutishwa au wapo katika hali ya kujihami, basi, kizuizi cha akili kinaongezeka na kinazuia kujifunza lugha kutokea. Kadiri wanafunzi wanapojisikia urahisi, kutiwa moyo, na kuamini kuwa mafanikio yanawezekana kwao, ndivyo watakavyoingiza lugha zaidi ndani. Hadi sasa, njia kuu ya mtu kujifunza Kiebrania kwa njia hii imekuwa kusoma huko Israeli kwa miezi au miaka. Lakini tunapaswa kukumbuka kuwa mshtuko wa utamaduni, chakula cha kigeni, gharama kubwa ya maisha, kuikosa familia nyumbani, kumzoea mwanachumba mwingine anayeishi naye, na kulazimika kupitia mazingira mapya ya kuongea Kiebrania cha kisasa (pamoja na Kiebrania cha Biblia darasani) hivi vyote vinaweza kuongeza msongo mkubwa wa mawazo, ambao utapelekea kuzuia mchakato wa kujifunza lugha. Wakati mwingine watafsiri wa Biblia kutoka nchi nyingine wanapambana na maisha katika Israeli, sio kwa sababu ya ubora wa programu yao au matunzo wanayopata kutoka kwa walimu, lakini ni kwa sababu tu lazima wazoee vitu vingi vipya kwa mara moja na wanazikosa familia zao.
Kwa hivyo swali letu ni kwamba, tunawezaje kuwatumikia vizuri kaka na dada zetu? Jibu ni: wape fursa ya kujifunza kutoka kwa faraja ya nyumba zao wenyewe. Video za bure ambazo unaweza kurudisha nyuma na kurudia vile vile unavyohitaji, kwa kasi yako mwenyewe haziogopehsi, hata kidogo! Hakuna wanafunzi wengine ambao wangeweza kuyacheka makosa yako, hakuna mwalimu ambaye angeweza kukosa uvumilivu (nimekuwa mmojawapo wa kukosa uvumilivu na wanafunzi!). Hauna wasiwasi juu ya shamba lako nyumbani, wala kumkosa mwenzi wako na watoto. Na ikiwa utapata nafasi ya kusafiri kwenda Israeli, tayari utakuwa na mwanzo mzuri kwa Kiebrania ili kuutumia vizuri wakati wako huko! Mwisho wa siku, tunatumaini video zetu zitalitumikia vizuri Kanisa la ulimwengu na kusawazisha fursa zilizopo ili kila mtu apate nafasi sawa, isiyo na msongo wa mawazo ya kujifunza Kiebrania cha kibiblia. Na tunawalika wengine wanaofundisha njia hii kujiunga nasi katika kufanya rasilimali nyingine za Data Inayoeleweka zipatikane bure!
Tunapendekeza sana kutazama video tatu zifuatazo za Stephen Krashen mwenyewe akielezea sayansi na nadharia ya njia tunayotumia, na pia kanuni zaidi za kufanikiwa katika upatikanaji wa lugha. Ingawa video ni za zamani, maudhui yaliyomo bado yanafaa na yanasaidia leo kama ilivyokuwa hapo awali. Kwa wale ambao wangependelea kusikiliza sauti zilizoingizwa katika mtandao (podcast) badala ya kutazama video, unaweza kusikiliza vipindi viwili vya Andrew juu ya kujifunza lugha ambavyo vinajumuisha na sauti ya Krashen anapofundisha hapa chini na zaidi.