Kwa nini Tafsiri ya Biblia?
Mathayo 28:19
Tume Kuu Inanuia Kazi ya Kutafsiri Biblia
Huwezi kuwafanya wanafunzi wa mataifa ikiwa wanafunzi hao hawawezi kupata neno la Mungu kwa lugha ambayo wanaelewa vizuri.
Warumi 10:14 pia inanuia tafsiri ya Biblia: “Je! Watamwaminije yeye ambaye hawajasikia habari zake? Je! Watasikiaje pasipo mtu anayehubiri kwao?” Huwezi kuhubiri injili kwa njia wazi inayovuta isipokuwa utumie lugha ambayo kikundi cha watu kinaielewa vizuri. Biblia iliyotafsiriwa inawezesha aina hiyo ya kuhubiri kufanikiwa na kuiingia mioyo kwa nguvu.
Ukuaji wa kiroho, mafundisho ya kweli, makanisa yenye afya, elimu ya kiteolojia, viongozi wanyenyekevu na wenye ujuzi, kupambana na mafundisho ya uwongo kama injili ya mafanikio – mambo hayo yote yanategemea kupata Biblia ambayo inawasiliana kwa uwazi na kwa usahihi katika lugha ya moyo wa mtu.
Takwimu za Kushangaza
Uhitaji
Ni Wakati kwa Mabadiliko ya Dhana
Toa Kiebrania
Watafsiri wengi wanapenda kujifunza Kiebrania kupitia njia ya mawasiliano, badala ya njia ya kisarufi ambayo watu wengi wasio wa ulimwengu wa magharibi wanaiogopa. Lakini kwa miaka wamelazimika kwenda Israeli kufanya hivyo, ambayo ni moja ya nchi ghali zaidi ya karibu na nchi zote nyingine ulimwenguni (zaidi hata ya Merikani, U.K., au Denmark). Hii inamaanisha kuwa walimu huko inawalazimu kuwatoza fedha nyingi wanafunzi wao ili kukusanya fedha nyingi kuweza kulipia gharama za programu zao. Pia mtafsiri mwenyewe lazima aache nyumba na familia yake kwa miezi kadhaa. Wakati mwingine pia inahitajika kwamba wazungumze Kiingereza. Wanaweza kuwa na akili nyingi, lakini hawana uwezo wa kulumudu gharama. Wengine wanaweza kupewa ufadhili, lakini hawawezi kuacha mashamba yao, huduma yao, au familia zao.
Sasa inakuja njia yetu ya bure, inayopatikana kila mahali. Tunatumaini watu wengi watajiunga nasi kutumia mfumo ambao hauzuiwa na hakimiliki au malipo.
Bei Rahisi na Njia Inayoweza Kubadilika badilika
Sisi wa Aleph na Beth tunaamini kuwa mafunzo ya Kiebrania ya Kibiblia yanapaswa kuwa 1) yanayoweza kubadilika badilika, 2) nafuu, na 3) yanapatikana. Ili kufikisha hitaji kubwa la kuwafundisha watafsiri zaidi ya 10,000, tunahitaji kitu ambacho kinaweza kunakiliwa kwa dijiti na kuenezwa kwa urahisi kwa maelfu ya watu. Kufundisha uso kwa uso ni bora, lakini ni njia ambayo haitoshelizi kulifikia hitaji la ulimwengu wote, kwa hivyo haipaswi kuwa chaguo pekee. Video zetu zinatoa njia mbadala ambayo haina kikomo cha idadi ya watu wanaoweza kuitumia kujifunza, kwa sababu zinapatikana hadharani bila vizuizi, na zina lugha moja (ambayo inamaanisha kuwa watu hawapaswi kujua lugha nyingine kama Kiingereza kujifunza ). Video zetu zinapatikana kwa unafuu, kwa sababu NI BURE. Na zinapatikana mahali popote duniani ikiwa mtu ana kifaa cha kuzitazama, hata mahali ambapo hakuna mtandao.
Kwa kuunda rasilimali hii tunatumaini kuwawezesha na kuwapa ujuzi walimu ambao wanataka kufundisha kwa njia hii katika sehemu yoyote ya ulimwengu. Wanaweza kutumia video zetu kuwaongoza watu katika kujifunza, na kujibu maswali kwa lugha ya mahali hapo.
יָבֵ֥שׁ חָצִ֖יר נָ֣בֵֽל צִ֑יץ וּדְבַר־אֱלֹהֵ֖ינוּ יָק֥וּם לְעֹולָֽם׃
-Isa 40:8